Katika hali isiyotarajiwa na wanafunzi wengi,yaani sawa na kumchekesha aliyenuna, Mwadili( DEAN OF STUDENTS) wa CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA KUMBUKUMBU YA ASKOFU MKUU MIHAYO TABORA(AMUCTA) ametoa tangazo la taratibu za mavazi kwa wanachuo wote yaani wake kwa waume. Kuanzia tarehe 18/06/2012 ambayo ni siku ya kuanza mitihani ya kumaliza semista ya II kwa mwaka wa masomo wa 2011/2012 kwa wanachuo hakuna ruhusa ya kuvaa jezi, kaptula/bukta nguo zozote za michezo isipokuwa kwa matukio husika T-shirt round collar, jeans, vimini, vibode tait, kata vitovu,...