Recent Posts

Sunday, January 6, 2013

PIGO JINGINE KWA TASNIA YA SANAA ZA MAIGIZO NA FILAMU NCHINI TANZANIA.

Posted by Unknown 11:05:00 PM, under | No comments

Msanii wa tasnia ya sanaa ya maigizo na filamu SAJUKI (JUMA KILOWOKO) alifariki dunia jana tarehe 02 Januari,2013 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Msanii huyo amefariki kwa upungufu wa damu baada ya kuugua muda mrefu. Kabla ya kifo chake marehemu alishakwenda nchini India kupata matibabu ya maradhi yanayomsumbua kupitia michango mbalimbali iliyochangwa na watanzania waliokuwa na mapenzi mema naye kupitia kampeni maalumu iliyofanywa na watu mbalimbali akiwemo mchekeshaji gwiji nchini Massanja Mkandamizaji wa Orijino Komedi nchini Tanzania. marehemu ameacha mke mmoja Wastara ambaye alikuwa anaigiza naye katika filamu na mtoto mmoja. Sajuki atakumbukwa kwa kazi zake nyingi za sanaa tangu akiwa kundi la Kaole Sanaa Group la jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.Katika fani ya filamu, marehemu ameigiza filamu kadha wa kadha kama vile MBONI YANGU, MCHANGA NA KENI pamoja na HERO OF THE CHURCH(SHUJAA WA KANISA) aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba na nyinginezo nyingi. Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh. January Makamba jana akihojiwa na kituo cha redio cha Clouds FM, alisema alimfahamu marehemu SAJUKI kama kijana aliyekuwa na malengo ya kufika mbali kisanaa na kimaisha kiujumla. Sajuki alikuwa na mpango wa kuandaa tamasha kubwa la kuwashukuru Watanzania wote waliomchangia michango mbalimbali ikiwemo fedha na sala zao kipindi chote alichokuwa anaumwa akiwa nchini na baada ya kwenda nchini India kupata matibabu ya maradhi yanayomsibu. Baba wa marehemu Mzee Kilowoko akihojiwa na vyombo vya habari alisema mwili wa marehemu utazikwa jijini Dar siku ya Ijumaa badala ya Songea mkoani Ruvuma kwenye asili ya babu zake ili kuruhusu watanzania wengi kushiriki mazishi ya Sajuki. Kifo hiki kimetokea ghala muda mfupi tu baada ya kuusheherekea mwaka mpya wa 2013, ikiwa ni siku chache kabla ya watanzania kusahau machungu ya kuondokewa na msanii mwingine wa filamu Shoro Millionea aliyefariki mwishoni mwa mwaka 2012 na kumbukumbu mbaya kabisa ya kuondokewa na nyota nyingine ya filamu Afrika marehemu Steven Kanumba Kazi yake Mola haina makosa mwenzetu ametutoka hatuna budi kumuombea alazwe mahala pema peponi AMINI.

0 comments:

Post a Comment

Tags

Total Pageviews

Labels