Recent Posts

Friday, January 18, 2013

SERIKALI YATOA SAA 24 KWA UONGOZI WA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA TPA ZIDI YA UBADHIRIFU WA MILIONI 450 FEDHA ZA KITANZANIA

Posted by Unknown 10:12:00 PM, under | No comments



Serikali imetoa masaa 24 kwa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA kutoa majibu ya uchakachuaji wa mkataba wa Mtambo wa kupakulia mafuta SBM na kusababisha ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 450.

Mkataba huo umedaiwa kubadilishwa kinyemela baada ya kuondolewa kipengele cha mzabuni cha kuendelea kuhudumia vipuri vya mtambo zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha kwa kipindi cha miaka miwili.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Mawaziri mbalimbali kwenye Mamlaka ya bandari TPA na hivyo kuzua kitendawili kikubwa kwa mawaziri hao.

Injinia Madeni Kipande ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA ambaye anajaribu kutegua kitendawili hicho.

Hata hivyo majibu yake hayakuridhisha viongozi hao na ndipo Waziri mwenye dhamana Dk. Harrison Mwakyembe akautaka uongozi wa TPA kukaa kikao na kuleta majibu ya kueleweka ifikapo jumatatu.

Mara ghafla linaibuka sakata lingine kuhusiana na kifaa cha kutambua idadi ya mizigo inayoingia na kutoka ambapo inabainika kuwepo kwa kifaa kimoja tu huku kifaa kingine kupelekwa Tanga kwa zaidi ya miaka miwili hali iliyochangia serikali kushindwa kutambua idadi ya mizigo inayoingia bandarini na kutoka.


Kufuatia hali hiyo ndipo Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda anawataka watumishi wa bandari kuwa waadilifu ili kuongeza ushindani wa soko kutokana na bandari kutegemewa kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa.


Miongoni mwa Mawaziri waliofanya ziara TPA ni Waziri wa Fedha na Uchumi Dk. William Mgimwa, Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na Naibu Waziri wa Nishati na Madini George Simba Chawene.

Mwisho.

0 comments:

Post a Comment

Tags

Total Pageviews

Labels