Chumvi kama madini muhimu katika kuongeza radha ya chakula yana madini joto muhimu kwa afya ya mwanadamu. Madini joto haya yakikosekana husababisha ugonjwa wa kuvimba shingo ROVU au kitaalamu wanauita GOITA. Je unajua chumvi inavyozalishwa kiasili huku kwetu Singida? Je unajua inatoka wapi au inatokana na nini?
Singida ni miongoni mwa sehemu kame nchini Tanzania yenye kupata mvua kiasi cha kuweza kuzalisha mazao kama alizeti, mtama, viazi nk.Pia mkoa huu ni maarufu kwa kuwa na mawe mengi hasa Singida Mjini"NG'ONGO" hali inayoufanya mkoa huu upendeze kwa jografia yake. Mchana jua kali na vumbi kiasi usiku baridi vilevile waulize wa jangwani wanafahamu maana kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
Singida imepakana na Tabora"Mboka" upande wa Magharibi, Dodoma upande wa Mashariki, Manyara upande wa Kaskazini, Mbeya upande wa Kusini.Umepitiwa na reli ya kati iliyojengwa na mkoloni tangu miaka 1910 na kuenendelea ina barabara kuu ya Arusha- Singida, Dodoma-Singida pamoja na Singida-Tabora kwa kiwango cha lami:"mkeka"
Mkoa una vyuo vya VETA, UHASIBU,SINGIDA TTC, KINAMPANDA TTC pamoja na shule kama MWENGE SEKONDARI(1967) iliyozinduliwa na hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere , pamoja na TUMAINI.
Mkoa huu pia una mabwawa ya maji ya Kindai na Singidani ambayo ni chanzo kikuu cha maji kwa wakazi wa Manispaa ya Siongida na viunga vyake.
Picha hii ni sehemu ya bwawa la Singidani.
Turudi kwenye jambo la msingi chumvi tazama picha zifuatazo uone uhondo wake.
Maji ya pembezoni mwa mabwawa haya yanachukuliwa pamoja na takataka za majani yaliyo kandokando ya mabwawa haya yenye chumvichumvi.
takataka hizi hukusanywa na kuwekwa kwenye ndoo yenye matundu yenye kuruhusu maji yenye chumvi kuvuja.
Ndoo hii/hizi huwekwa juu ya mawe yaliyosafishwa vizuri na kuwekewa kauzio kadogo kanakoweza kuzuia kutoroka kwa maji hayo na kuachwa yagande kwenye mawe hayo.
Kisha maji hayo ya chumvi huachwa yakauke kwenye mawe kwa siku kadhaa kabla ya chumvi kuvunwa kwa ajili ya matumizi.
chumvi huganda taratibu yategemea kiwango cha jua kilichopo na shughuli hii mara zote hufanywa kiangazi.
weupe wa pembeni ni chumvi iliyoanza kuganda.
chumvi huvunwa ikiwa nyeupe pee na si kama inavyoonekana pichani.
weupe huu pichani unaoonekana ni sehemu ya mabaki ya chumvi yaliyokutwa na mwandishi wa blog hii.
Hapa Bwana Chihimba(mwenye shati la khaki) akishangaa baadhi ya madimbwi ya chumvi na mwenyeji wake huko mkoani Singida.