Recent Posts

Monday, May 20, 2013

4 International Colleges & Universities

Posted by Unknown 4:27:00 PM, under | No comments

Sunday, May 12, 2013

TUHUMA ZA UFREEMASON KWA MFANYABIASHARA MAARUFU WA JIJIN DAR ES SALAAM- TANZANIA

Posted by Unknown 5:02:00 PM, under | No comments

Tuesday, January 22, 2013

UGUMU WA MAISHA NA MASLAHI DUNI YASABABISHA ASKARI KUPOTEZA MAISHA KWA AJALI AKISAFIRISHA MIRUNGI

Posted by Unknown 1:57:00 AM, under | No comments

ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha PC Samson (20) amefariki dunia akisafirisha mirungi. Kufariki kwa PC Samson kulitokea juzi katika eneo la Mdori mkoani Manyara baada ya kupata ajali ya gari alilokuwa akilitumia kusafirisha mirungi hiyo kutoka Arusha.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari eneo hilo la Mdori wilayani Babati zilieleza jana kwamba ajali hiyo ilitokea saa 12:30 asubihi.

Chanzo cha habari kilichoshuhudia tukio hilo kilisema kuwa gari hilo liliacha njia na kuanguka pembeni mwa barabara, hatua iliyosababisha shehena ya mirungi iliyobebwa kumwagika nje.

Wakati taarifa kutoka Mdori zikieleza hayo, mtoa taarifa mwingine kutoka Majengo Kata ya Elerai Arusha alidai kwamba gari hilo lilionekana saa 10 alfajiri likielekea barabara kuu ya Arusha - Babati.

Hata hivyo chanzo hicho kutoka Arusha nacho kilieleza kwamba shehena hiyo ya mirungi ilikuwa mali ya mmoja wa wafanyabiashara wa mirungi jijini hapa (kwa sasa jina linahifadhiwa).

Kamanda wa Polisi Manyara, Akili Mpwapwa alikiri tukio hilo lilitokea saa 12:30 asubuhi eneo la Mdori wilayani Babati. Alilitaja gari lililotumika kusafirisha mirungi hiyo kuwa ni Toyota Carrina namba T. 588 AUW ambalo linadaiwa kuacha njia na kupinduka kutokana na mwendo kasi.
Pamoja na kifo cha PC Samson mtu mwingine anayedaiwa kuwa dereva wa gari hilo Hussein Bakari (20-30) ambaye ni mkazi wa Arusha naye alifariki dunia papo hapo.

Taarifa tulizozipata zinadai kwamba askari huyo alikuwa likizo.

Hivi karibuni Jeshi la Polisi mkoani Arusha lilikamata shehena ya mirungi ya thamani ya Sh milioni 40 ikiwa imejazwa kwenye gari ya Canter wilayani Longido.

ESCAPE FROM SOBIBO ATOROKA GEREZANI NA KUVUA NGUO ASIKAMATWE NA POLISI

Posted by Unknown 1:22:00 AM, under | No comments


Na Nassor Wazambi (facebook) Tabora Manispaa

Mwananchi mmoja kwa kushirikiana na askari wa kikosi cha kuzuia ghasia FFU mjini Tabora wamefanikiwa kumkamata mfungwa mmoja wa gereza la mahabusu Tabora wakati akifanya jaribio la kutoroka akiwa amevua nguo na kubakia uchi wa mnyama.
Mfungwa huyo ambaye anafahamika kwa jina la Jonas Oscar(25)imedaiwa kuwa mnamo majira ya mchana siku ya tarehe 14 januari 2013 alifanya jaribio hilo wakati akiwa kwenye kazi za bustanini na wafungwa wenzake.
Hata hivyo wakati akiwa ameanza safari hiyo ya kukwepa kifungo cha mwaka mmoja ambacho ameanza kukitumikia mapema mwaka huu,mfungwa huyo Jonas aliibukia katika kambi ya Jeshi la Polisi iliyoko jirani na gereza hilo la mahabusu hatua ambayo ilisababisha kuonwa mapema kwakuwa alionekana kuwa ni mtu wa ajabu kwa kukimbia akiwa uchi wa mnyama.
Aidha katika hatua nyingine mfungwa huyo amefikishwa mahakama ya wilaya ya Tabora,mbele ya hakimu Mheshimiwa Magori na kukabiliwa kwa kosa la kutoroka chini ya ulinzi halali kinyume cha sheria namba 16 kifungu cha 116 ya mwaka 2002,ambapo alihukumiwa kutumikia adhabu kwenda jela kwa kifungo cha miezi 16,adhabu ambayo ameanza kuitumikia mara moja.
Awali Jonas Oscar imedaiwa kuwa alikuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja akiwa ni mfungwa No.02,2013 katika Gereza la mahabusu Tabora mjini baada ya kupatikana na hatia ya kutishia kumuua baba yake mdogo huko katika wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Mwananchi mmoja kwa kushirikiana na askari wa kikosi cha kuzuia ghasia FFU mjini Tabora wamefanikiwa kumkamata mfungwa mmoja wa gereza la mahabusu Tabora wakati akifanya jaribio la kutoroka akiwa amevua nguo na kubakia uchi wa mnyama.
Mfungwa huyo ambaye anafahamika kwa jina la Jonas Oscar(25)imedaiwa kuwa mnamo majira ya mchana siku ya tarehe 14 januari 2013 alifanya jaribio hilo wakati akiwa kwenye kazi za bustanini na wafungwa wenzake.
Hata hivyo wakati akiwa ameanza safari hiyo ya kukwepa kifungo cha mwaka mmoja ambacho ameanza kukitumikia mapema mwaka huu,mfungwa huyo Jonas aliibukia katika kambi ya Jeshi la Polisi iliyoko jirani na gereza hilo la mahabusu hatua ambayo ilisababisha kuonwa mapema kwakuwa alionekana kuwa ni mtu wa ajabu kwa kukimbia akiwa uchi wa mnyama.
Aidha katika hatua nyingine mfungwa huyo amefikishwa mahakama ya wilaya ya Tabora,mbele ya hakimu Mheshimiwa Magori na kukabiliwa kwa kosa la kutoroka chini ya ulinzi halali kinyume cha sheria namba 16 kifungu cha 116 ya mwaka 2002,ambapo alihukumiwa kutumikia adhabu kwenda jela kwa kifungo cha miezi 16,adhabu ambayo ameanza kuitumikia mara moja.
Awali Jonas Oscar imedaiwa kuwa alikuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja akiwa ni mfungwa No.02,2013 katika Gereza la mahabusu Tabora mjini baada ya kupatikana na hatia ya kutishia kumuua baba yake mdogo huko katika wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Friday, January 18, 2013

SERIKALI YATOA SAA 24 KWA UONGOZI WA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA TPA ZIDI YA UBADHIRIFU WA MILIONI 450 FEDHA ZA KITANZANIA

Posted by Unknown 10:12:00 PM, under | No comments



Serikali imetoa masaa 24 kwa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA kutoa majibu ya uchakachuaji wa mkataba wa Mtambo wa kupakulia mafuta SBM na kusababisha ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 450.

Mkataba huo umedaiwa kubadilishwa kinyemela baada ya kuondolewa kipengele cha mzabuni cha kuendelea kuhudumia vipuri vya mtambo zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha kwa kipindi cha miaka miwili.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Mawaziri mbalimbali kwenye Mamlaka ya bandari TPA na hivyo kuzua kitendawili kikubwa kwa mawaziri hao.

Injinia Madeni Kipande ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA ambaye anajaribu kutegua kitendawili hicho.

Hata hivyo majibu yake hayakuridhisha viongozi hao na ndipo Waziri mwenye dhamana Dk. Harrison Mwakyembe akautaka uongozi wa TPA kukaa kikao na kuleta majibu ya kueleweka ifikapo jumatatu.

Mara ghafla linaibuka sakata lingine kuhusiana na kifaa cha kutambua idadi ya mizigo inayoingia na kutoka ambapo inabainika kuwepo kwa kifaa kimoja tu huku kifaa kingine kupelekwa Tanga kwa zaidi ya miaka miwili hali iliyochangia serikali kushindwa kutambua idadi ya mizigo inayoingia bandarini na kutoka.


Kufuatia hali hiyo ndipo Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda anawataka watumishi wa bandari kuwa waadilifu ili kuongeza ushindani wa soko kutokana na bandari kutegemewa kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa.


Miongoni mwa Mawaziri waliofanya ziara TPA ni Waziri wa Fedha na Uchumi Dk. William Mgimwa, Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na Naibu Waziri wa Nishati na Madini George Simba Chawene.

Mwisho.

Monday, January 14, 2013

JERRY SILAHA AWASHA MOTO MBEYA AWATAKA UVCCM KUWA MACHO NA WANAOTAKA KUHUJUMU CHAMA KWA MASLAHI YAO

Posted by Unknown 11:42:00 PM, under | No comments



 JERRY SILAA AKIFUNGUA SEMINA YA SIKU MBILI YA VIONGOZI WA UVCCM MKOA WA MBEYA. KUSHOTO  NI AMAN KAJUNA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA MBEYA
KATIBU WA CCM WILAYA YA MBEYA AKIMWAGA SERA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA WAKAZI WA NZOVWE MBEYA 
AMAN KAJUNA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA MBEYA AKIMKARIBISHA JERRY SILAA AONGEE NA WANANCHI WA NZOVWE MBEYA
JERRY SILAA AKIONGEA NA WANANCHI WA NZOVWE MBEYA
VIJANA WA CCM WAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA JERRY SILAA

DOGO AKIMSIKILIZA SILAA


MEYA wa Ilala , Jerry Slaa, amesema kuwa licha ya umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kuonekana kuwa nguzo ndani ya chama hicho, lakini ndiyo jumuiya inayongoza kwa migawanyiko na makundi ndani ya chama hicho, inayochochewa na watu toka nje.


Slaa ambaye pia, ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), kutoka wilaya ya Ilala, amesema kuwa hali hiyo inakiweka rehani chama hicho, hivyo kuwataka vijana hao wabadilike na kuacha kufanya siasa za mtu, bali wafanye siasa za chama, kwani hiyo ndio suluhu itakayoiwezesha chama hicho kurudisha imani kwa jamii.


Alitoa kauli hiyo jana, Jijini hapa, wakati akifungua semina ya siku mbili ya viongozi 60 wa jumuiya hiyo, kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya, iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi kwa lengo la kwenda kukijenga chama baada ya kumalizika uchaguzi wa ndani.


Alisema licha ya kwamba CCM bado inaaminiwa kwa kiasi kikubwa na jamii, lakini bado kuna mambo muhimu ambayo chama hicho na jumuiya zake, kinapaswa kuendelea kuyafanya ili kuendelea kukiimarishaya na kujenga imani zaidi ndani ya jamii.

Hata hivyo , alisema wakati vijana hao wakifurahia kupata nafasi za kushika madaraka mbalimbali, lakini pia wanapaswa kufikiria zaidi wajibu wao kuanzia katuika sehemu wanazotoka hadi kwenye nyadhifa walizoshika, ikiwemo kusimamia ipasavyo utekelezaji wa ilani ya chama hicho.


“Wewe kama kiongozi unapaswa kujiuliza ni kwa kiwango gani umetimiza wajibu wako huko uliko (sehemu wakaoishi), lakini pia ni kiwango gani umezisimamia halmashauri katika kutekeleza ilani ya chama” alisema Slaa.

Alisema kazi kubwa ya jumuiya hiyo na wana CCM kwa ujumula ni kuunganisha nguvu zao kwa pamoja ili kuendelea kukijenga chama ili kiaminiwe na wananchi na hatimaye kuendelea kupewa dhamana ya kuongoza dola.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi huo wa semina elekezi kwa viongozi wa jumuiya hiyo, Mwenyekitti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, alisema vijana nchini wakiwemo wa CCM wanapaswa kuwa jicho la mabadiliko hapa nchini.


Aliongeza kuwa vijana nchini wanatakiwa kuacha kuendesha mambo na mipango yao kwa mazoea badala yake watekeleze hayo kulingana na mabadiliko ya ulimwengu wa sasa na mahitaji ya jamii.

Baada ya kufungua semina hiyo ya siku mbili, MNEC huyo, alifanikiwa pia kukutana na viongozi mbalimbali wa chama hicho na alitarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika eneo la Nzovwe Jijini hapa.

Na Moses Ng’wat,  picha na Mbeya yetu

Sunday, January 6, 2013

P SQUARE UGANDA,WAAPA KUTOKANYAGA TENA NCHI HIYO

Posted by Unknown 11:44:00 PM, under | No comments

Licha ya kupiga show ya nguvu mjini Kampala, Uganda mwezi uliopita, wasanii wa kundi la P-Square wamedaiwa kuapa kutokanyaga tena ardhi ya Uganda kwaajili ya show. Uamuzi huo wameuchukua baada ya kudaiwa kushikiliwa kwa masaa kwenye hoteli ya nyota 5 waliyokuwa wamefikia kwa kushindwa kulipa bili. Waandaji wa show hiyo walikataa kulipa bili hiyo kutokana na kuwa kubwa mno.Kwa mujibu wa vyanzo, mapacha hao Peter na Paul walisaini mkataba na mapromota hao na walilipwa gharama ya kufanyia show huku zile za malazi na usafiri zikiachwa. Hata hivyo kulikuwa na kiwango cha mwisho ambacho wasanii hao walitakiwa kukitumia pale walipofikia lakini walizidisha na hivyo waandaji kuwataka walipe wenyewe na hivyo kuleta mgogoro mkubwa. Wasanii hao wa Alingo walichukizwa na kitendo hicho na sasa wameahidi kutoenda nchini Uganda tena!!

PIGO JINGINE KWA TASNIA YA SANAA ZA MAIGIZO NA FILAMU NCHINI TANZANIA.

Posted by Unknown 11:05:00 PM, under | No comments

Msanii wa tasnia ya sanaa ya maigizo na filamu SAJUKI (JUMA KILOWOKO) alifariki dunia jana tarehe 02 Januari,2013 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Msanii huyo amefariki kwa upungufu wa damu baada ya kuugua muda mrefu. Kabla ya kifo chake marehemu alishakwenda nchini India kupata matibabu ya maradhi yanayomsumbua kupitia michango mbalimbali iliyochangwa na watanzania waliokuwa na mapenzi mema naye kupitia kampeni maalumu iliyofanywa na watu mbalimbali akiwemo mchekeshaji gwiji nchini Massanja Mkandamizaji wa Orijino Komedi nchini Tanzania. marehemu ameacha mke mmoja Wastara ambaye alikuwa anaigiza naye katika filamu na mtoto mmoja. Sajuki atakumbukwa kwa kazi zake nyingi za sanaa tangu akiwa kundi la Kaole Sanaa Group la jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.Katika fani ya filamu, marehemu ameigiza filamu kadha wa kadha kama vile MBONI YANGU, MCHANGA NA KENI pamoja na HERO OF THE CHURCH(SHUJAA WA KANISA) aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba na nyinginezo nyingi. Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh. January Makamba jana akihojiwa na kituo cha redio cha Clouds FM, alisema alimfahamu marehemu SAJUKI kama kijana aliyekuwa na malengo ya kufika mbali kisanaa na kimaisha kiujumla. Sajuki alikuwa na mpango wa kuandaa tamasha kubwa la kuwashukuru Watanzania wote waliomchangia michango mbalimbali ikiwemo fedha na sala zao kipindi chote alichokuwa anaumwa akiwa nchini na baada ya kwenda nchini India kupata matibabu ya maradhi yanayomsibu. Baba wa marehemu Mzee Kilowoko akihojiwa na vyombo vya habari alisema mwili wa marehemu utazikwa jijini Dar siku ya Ijumaa badala ya Songea mkoani Ruvuma kwenye asili ya babu zake ili kuruhusu watanzania wengi kushiriki mazishi ya Sajuki. Kifo hiki kimetokea ghala muda mfupi tu baada ya kuusheherekea mwaka mpya wa 2013, ikiwa ni siku chache kabla ya watanzania kusahau machungu ya kuondokewa na msanii mwingine wa filamu Shoro Millionea aliyefariki mwishoni mwa mwaka 2012 na kumbukumbu mbaya kabisa ya kuondokewa na nyota nyingine ya filamu Afrika marehemu Steven Kanumba Kazi yake Mola haina makosa mwenzetu ametutoka hatuna budi kumuombea alazwe mahala pema peponi AMINI.

MSUGUANO NDANI YA CHADEMA WANACHAMA WAANZA KUFUKUZANA NA KUVUANA UANACHAMA

Posted by Unknown 10:59:00 PM, under , | No comments

TAARIFA HII IMETOKA MOJA KWA MOJA KWENYE MIKONO YA BAADHI YA WAJUMBE WA KIKAO CHA KAMATI TENDAJI YA VIJANA (BAVICHA) Ndugu Wanajukwaa, Taarifa za kuvuliwa uanachama kwa Juliana Shonza (Makamu Mwenyekiti BAVICHA), Mtela Mwampamba na Habib Mchange ni za kweli! Hatua hii ilifikiwa jana na kikao cha kamati tendaji ya BAVICHA iliyokutana pale Ukumbi wa Mbezi Garden majira ya Saa sita na nusu Mchana. Kikao hiki kimsingi hakikuweka wazi ajenda za kwenda kujadili uanchama wa wahusika hapo juu (Pitia taarifa ya Tumaini Makene hapa JF kuhusu kikao hicho) licha ya wahusika hao hapo juu kualikwa kuhudhuria kikao hicho. Wajumbe walioalikwa kwa ajili ya kikao hiki ni kama wafuatao: (Hawa wahusika si wajumbe wa kikao cha kamati tendaji BAVICHA) 1. Ben Saanane 2. Chacha Hatari 3. Habib Mchange 4. Mtela Mwampamba 5. Gwakisa Burton Mwakasendo. Hao wajumbe hapo juu walihojiwa na kamati tendaji kila mmoja kwa nafasi yake na mashitaka yake mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la vijana Ndugu John Heche na katibu Deo Munishi. Naomba kuyaweka mahojiano kama ifuatavyo, (mahojiano yalianza kufanyika saa tatu na nusu usiku). Ben sanaane alihojiwa kwanini ametoa shutuma kali mitandaoni kwa viongozi wake wa juu (Zitto)? Majibu ya msingi ya Ben Saanane yalikuwa ni kwamba aliamua kufanya vile kwasabu ya kukilinda chama na viongozi wake wasihafuliwe mitandaoni na vijana aliowataja ni 'Masalia'. Swali likaja; yeye haoni kama alikuwa anamchafua Zitto ambaye ni kiongozi wa chama? Jibu lake lilikuwa ni kuomba radhi amekosea. Mtela mwampamba alihojiwa kwa kuulizwa mashitaka mawili. Moja ni kwanini anampinga Dr. Slaa kuwa anamiliki kadi ya CCM na pili kwanini alimkashifu Dr. Slaa hapa JF kwa kutumia 'Verified Account'Majibu ya Mwampamba ni kama ifuatavyo:Kwanza alianza kwa kuomba kubadilishiwa mwenyekiti wa kikao kwasababu hana imani naye. Kwanini hana imani naye? Ni kwa sababu wana 'conflict of interest' kwenye siasa (kuanzia kwenye uchaguzi wa BAVICHA) hawaelewani hivyo anaamini haki haitatendeka endapo Heche atasimamia mahojiano yale. Mjumbe mmoja (mwenyekiti Arusha) akanyoosha mkono kwa kusema asiwasumbue wapo kazini. Mwampamba akajibu, hata mbunge wa Arusha Godbles Lema aliomba kubadilishiwa jaji kwenye kesi yake kwasababu alikuwa hana imani naye. Mwampamba akaongeza kwa kusema Ibara ya 18 na 19 ya katiba mama ya nchi inampa uhuru wa kuchagua nani wakusikiliza maoni yake na haki ikatendeka. Mjumbe mwingineakasimama akasema kuwa yeye ameacha kata yake na kuja kusikiliza, Mwampamba unatusumbua. Mwampamba akamjibu mimi nimeacha wanachi 32,000 kule Mbozi jimboni (alikogombea ubunge mwaka 2010) wanaonitegemea nimekuja hapa, wewe unataka kusema ndio unajua sana kazi? Kilichotokea: Bwan John Heche akagadhabika na kuamuru mabaunsa sita (6) wakiongozwa na Baunsa wa Mbowe anayejulikana kwa jina la 'Swai' wamtoe nje. Mwampamba alitolewa nje kwa nguvu, akatoka!HABIB MCHANGE:Yeye alikuwa na shitaka la kuwakashifu viongozi mitandaoni. Habib Mchange akahoji kwa mwenyekiti wa kikao. Kwanza alihoji uhalali wa kikao, kwasababu kile kikao kikatiba hakipo kwasababu hakuna makatibu wa baraza la vijana ni kikao cha wenyeviti tu? Pia, akaomba aelezwe ameitwa kama nani kwenye kikao kile? Pia akaomba apewe mashitaka yake yenye uthibitisho wa yeye kuhusika na hayo wanayo yasema. Mwenyekiti kwa hasira akaamuru mabaunsa wamtoe Mchange nje! Mchange kwa ustaarabu akatoka nje.Gwakisa Burton:Yeye alikuwa na mashitaka mawili la kumpinga Dr. Slaa kuwa na kadi mbili ya CHADEMA na CCM pamoja na kumpinga Sugu Mbunge wa Mbeya mjini (CHADEMA). Bila kuchelea Gwakisa akakili kweli alimpinga Dr. Slaa kwa kumiliki kadi mbili, Pia alikili alimpinga Sugu kwasababu wanatofautiana kimawazo (ikumbukwe Gwakisa alitolewa kwenye kura za maoni jimbo la Mbeya Mjini ili Sugu apitishwe kuwa mgombea). Alichokifanya mwenyekiti John Heche palepale akaamuru kumsamehe Gwakisa na kupewa onyo kali la kutorudia tena kuwapinga viongozi wake. Ndugu wana JF, Kikao kilimalizika mnano saa 5 na dakika 46 usiku. Maazimio ya kikao kile ni kuwavua uanachama wahusika watatu hapo juu. UTATA ULIPOJITOKEZA: Kimsingi katiba hairuhusu kabisa na haiwapi mamlaka BAVICHA kufukuza uanachama mtu yeyote. Kwenye katiba hakuna sehemu kamati tendaji inapewa nafasi ya kuhoji na kufukuza wanchama ndani ya chama. Pia, Juliana Shonza atavuliwajwe uongozi na kamati tendaji wakati katiba inaeleza wazi kuwa mkutano mkuu utaitishwa lilikumvua uongozi kwa sababu yeye alichaguliwa na mkutano mkuu? HATUA ALIYOICHUKUA FREEMAN MBOWE: Nimetoka makao makuu ya CHADEMA muda huu pale Kinondoni, wameandaa toka asubuhi eneo, ambapo palitakiwa pafanyike Press Conference na vyombo vya habari kuhusu maazimio ya jana kwenye kikao. Freeman Mbowe amezuia hatua hiyo ya kutangaza maazimio hayo kwa sababu BAVICHA hawana mamlaka ya kumuwajibisha mwanachama yeyote, Kinachotakiwa BAVICHA kukifanya ni kupeleka mapendekezo yao kamati kuu ya CHADEMA taifa ndiko maamuzi yote yatafanyika. Kwa maana hiyo John Heche na Mbowe wapo kwenye msuguano mkali,Kutokana na kwamba hili swala likifika kamati kuu litakwend akinyume na wanavyotaka.wajumbe wengi wa kamati kuu wanaendesha mamuzi yao kiutuuzima,bila hisia na kikatiba. Pia uzito wa makosa haya haupelekei kupoteza vijana hawa wenye umuhimu mkubwa kwenye majimbo yao na kwenye chama.KUHUSU JULIANA SHONZA:Yeye hakufika kwenye kikao kile kutokana na kutokuwepo jijini Dar es Salaam na taarifa kuchelewa kumfikia. Hivyo walishindwa kufanya mahojiano naye na kumpatia mashitaka yake. HALI NDANI YA KIKAO ILIVYOKUWA: Wajumbe walionekana kuandaliwa ipasavyo kisaikolojia kwaajili ya kuwakabili Mwampamba na Mchange. Kwa sababu walipoingizwa kwenye ukumbi wa kikao kila mmoja alitengewa kiti chake na kukabishiwa mabaunsa 6 kwa ulinzi. Muda wote Mwampamba na Mchange walikuwa kwenye ulinzi mkali sana. Waalikwa wengine kama Saanane na Gwakisa na hatari walikwa hawana ulinzi, wapo free. MWISHO: Hii ndio CHADEMA, kuna uwezekano wa wanachama wengi wakafukuzwa kwa kupigiwa simu tu bila katiba kufuatwa. Pia kufukuza wanachama ndio last solution kwa kulea vijana? SOURCE:JAMIIFORUM/Jukwaa la siasa