ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia
(FFU) mkoani Arusha PC Samson (20) amefariki dunia akisafirisha
mirungi. Kufariki kwa PC Samson kulitokea juzi katika eneo la Mdori
mkoani Manyara baada ya kupata ajali ya gari alilokuwa akilitumia
kusafirisha mirungi hiyo kutoka Arusha.
Taarifa
kutoka vyanzo mbalimbali vya habari eneo hilo la Mdori wilayani Babati
zilieleza jana kwamba ajali hiyo ilitokea saa 12:30 asubihi.Chanzo
cha habari kilichoshuhudia tukio hilo kilisema kuwa gari hilo liliacha
njia na kuanguka pembeni mwa barabara,...