Recent Posts

Friday, October 26, 2012

NA HAYA NDIYO MANENO YA AFANDE SELE MGOMBEA UBUNGE MTARAJIWA JUU YA NAIBU WAZIRI WA ELIMU BW. PHILIP MULUGO KUHUSU TANZANIA NI MUUNGANO WA KISIWA CHA PEMBA NA ZIMBABWE HUKO AFRIKA KUSINI

Posted by Unknown 9:45:00 PM, under | No comments



Na Millard Ayo
.
Baada ya Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Philipho Mulugo kuomba radhi kwa wote waliomfikiria vingine baada ya kuzungumza kwenye mkutano Afrika Kusini kwamba Tanzania ni muungano wa Pemba na Zimbabwe msanii wa bongofleva Afande Sele ametoa maoni yake.
Sele ambae ameahidi kugombea ubunge wa Morogoro mjini 2015 huku akisisitiza kwamba atakua kwenye chama pinzani na sio CCM namkariri akisema “ni jambo lisilofikirika licha ya dhamana ya uwaziri aliyonayo muheshimiwa Waziri inasikitisha, kitu kibaya ni kwamba yeye ni naibu Waziri wa elimu na hilo swala linahusiana na maswala ya kitaaluma, nchi imepata uhuru mwaka gani, imeingia kwenye muungano mwaka gani, imeungana na nchi gani”
“Inasikitisha kwa sababu ni waziri alafu ni Waziri wa Elimu na swala lenyewe linahusiana na swala la kielimu, kama waziri mwenye dhamana ya elimu anashindwa kutambua basi ndio maana wanasema kwamba mtandao mzima wa serikali yetu basi mara nyingi haufanyi kile ambacho watu wanategemea kwamba kingefanywa vizuri, ndio maana inasainiwa mikataba mibovu kwa sababu mtu anawekwa kwenye  nafasi ambazo hakustahili kuwepo” – Afande Sele
“Hana taaluma, hana uwezo wa kuwa na cheo au mamlaka flani… anapewa kwa sababu ya undugu, urafiki pengine na wale wenye ngazi za juu zaidi ndio wanaochangia kuwa na aina ya mawaziri wa aina ya huyu naibu waziri anashindwa kujua tarehe ya kuungana kwa nchi yetu, kwa hiyo ni mmomonyoko ambao umeanzia juu ambapo ushindi wa yote ni kuivunja nyumba na kujenga upya… swala la kujua tarehe ya uhuru, tarehe ya muungano swala la utaifa kama hilo halihitaji kusema eti mashine iweke sawa au mashine igeuze hata ukikosea maandishi mimi siwezi kukosea kama wewe, hana upeo hana elimu hastahili kuwepo hapo alipo, hata mtoto kama mwanangu Tunda hawezi kukosea jambo kama hilo” – Afande Sele

HUYU NDIO DJ MTANZANIA AMBAE AMEFANYA KAZI NA HAWA MASTAA WA DUNIA KAMA CHRIS BROWN IRELAND.

Posted by Unknown 9:33:00 PM, under | No comments

Na Millard Ayo


Dj Frank Jez ni mtanzania ambae aliondoka Tanzania kwenda Ireland kusoma miaka ya 90 na baadae akaamua kuishi huko na kuanza kuwa Dj, mpaka sasa ameshaandaa na kufanya show na mastaa mbalimbali wa muziki duniani.
Dj Frank na B.O.B

.
.
Dj Frank Jez na Akon
Na Chris Brown.
.
.
.
Na Chipmunk
Na Tinie Tempa
.
.
Na Wyclef
Na Trey Songs
Na Neyo
Na Rick Ross.
.
Mtoto wa Dj Frank Jez na Jason Derulo.
Na Diddy.
Na The Game
Na Mindless Behaviour.

Wednesday, October 17, 2012

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO, STORI KUBWA NI MCHEZAJI SOKA KWENYE TUHUMA ZA MAUAJI YA KAMANDA WA POLISI MWANZA.

Posted by Unknown 9:09:00 AM, under | No comments

Magazeti haya ni kwa msaada wa www.millardayo.com


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

DK.ANTONY DIALLO ASHINDA UENYEKITI WA CCM MWANZA KWA KURA NYINGI UENYEKITI CCM MKOA

Posted by Unknown 8:50:00 AM, under | No comments



0
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza Anthony Diallo(mwenye mashada-maua) ndiye  aliyeibuka mshindi kwa kura 611 katika wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, amemshinda aliekua mwenyekiti wa chama hicho Clement Gregory Mabina aliepata kura 328 (Picha kutoka kwa gsengo.blogspot.com habari na  MillardAyo in News 17th 0ct,2012 )

HONGERENI WAZANZIBARI marufuku ya Pombe,Sigara Na Ukahaba Zanzibar

Posted by Unknown 1:53:00 AM, under | No comments


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku biashara ya ukahaba, matangazo yote ya pombe na uvutaji wa sigara katika mikusanyiko ya watu katika visiwa vya Unguja. Hayo yamebainika kufuatia marekebisho ya kifungu cha sheria cha 112, cha mswada wa sheria kuhusiana na hifadhi na usimamizi wa vihatarishi vya afya ya jamii na afya ya mazingira na mambo yanayohusiana na hayo iliyopitishwa ndani ya Baraza la Wawakilishi jana.Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji aliwaambia wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba kutokana na michango mingi ya wajumbe kutaka suala la matangazo ya pombe, uvutaji wa sigara, na biashara ya ukahaba vipigwe marufuku, serikali imekubaliana na maoni ya wajumbe hao. Waziri Duni amesema, kuanzia sasa kwa mujibu wa sheria hiyo itakuwa ni marufuku kutangaza au kushajiisha matangazo ya pombe kwa kutumia njia mbalimbali zikiwemo ufadhili au matamasha ya muziki na starehe katika visiwa hivyo. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman alisema anakubaliana na maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuondoa kabisa matangazo ya pombe na kwamba serikali imefanya vyema, kwani hivi sasa Shirika la Afya Duniani WHO, Umoja wa Ulaya EU na baadhi ya nchi ikiwemo Sweden tayari zimezuia matangazo ya pombe na Zanzibar kufuata sheria hiyo ni jambo la busara.

WAKUTANAPO WAKUU WA NCHI>>>>>>SULTANI QABOOS WA OMAN AMTUNUKU NISHANI YA HESHIMA RAIS JAKAYA KIKWETE

Posted by Unknown 1:23:00 AM, under | No comments


Sultani wa Oman,Qaboos bin Said Al Said (kulia)  akimtunuku Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Nishani ya juu ya heshima ya Taifa la Oman wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake jana jioni katika kasri ya  AL Alam jijini Muscat Oman.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya AL Alam jijini Muscat Oman jana jioni muda mfupi kabla ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa kwa heshima yake.
Sultan Qaboos bin Said Al Said akimpongeza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku nishani ya juu ya heshima ya Taifa la Oman jana jioni katika kasri ya AL Alam, Jijini Muscat Oman jana jioni .Rais Kikwete aliwasili nchini Oman jana jioni kwa ziara rasmi ya siku tatu.
Picha na Freddy Maro.HABARI KWA MSAADA WA aloyson.blogspot.com

BREAKING NEWS: HATARIIIIIIIIIIIII............... Bweni lanusurika kuteketea katika chuo cha UTUMISHI WA UMMA (TPSC) TABORA

Posted by Unknown 1:10:00 AM, under | No comments


 Hiki ndicho chumba moto ulipoanzia
Bweni hilo la wasichana maarufu kwa jina la Shaaban Roberth limenusurika kuteketea kwa moto usiku huu kwa kuanza kuungua moja ya chumba kilichopo flow ya juu katika bweni hilo, ikiwa dalili za awali zinaonesha chazo ni shoti ya umeme kwenye switch ya ukutani (Wall Switch Socket).
Juhudi za kuokoa zilifanikiwa mapema na kuzuia moto huo kuendelea kuteketeza bweni hilo, zana za fire extinguisher zilitumika na hatimaye kuokoa athari ambazo zingetokea. Hata hivyo kikosi cha zimamoto hakikuchelewa kufika eneo la tukio.
Pia mmoja kati ya wanachumba hicho alizimia baada ya tukio hilo kutokea.
HABARI: KWA MSAADA WA ALOYSON.BLOGSPOT.COM

Friday, October 5, 2012

MARIO BALOTELLI ARUDIANA NA MPENZI WAKE WA ZAMANI

Posted by Unknown 12:17:00 AM, under | No comments


Mchezaji wa Manchester City Mario Balotelli akiwa na mpenzi wake Raffaella mwenye ujauzito, waliachana April 2012 baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa mwaka mmoja, sasa hivi wamerudiana tena.
.
.