Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku biashara ya ukahaba, matangazo
yote ya pombe na uvutaji wa sigara katika mikusanyiko ya watu katika
visiwa vya Unguja. Hayo yamebainika kufuatia marekebisho ya kifungu cha
sheria cha 112, cha mswada wa sheria kuhusiana na hifadhi na usimamizi
wa vihatarishi vya afya ya jamii na afya ya mazingira na mambo
yanayohusiana na hayo iliyopitishwa ndani ya Baraza la Wawakilishi
jana.Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji aliwaambia wajumbe wa Baraza
la Wawakilishi kwamba kutokana na michango mingi ya wajumbe kutaka
suala la matangazo ya pombe, uvutaji wa sigara, na biashara ya ukahaba
vipigwe marufuku, serikali imekubaliana na maoni ya wajumbe hao. Waziri
Duni amesema, kuanzia sasa kwa mujibu wa sheria hiyo itakuwa ni marufuku
kutangaza au kushajiisha matangazo ya pombe kwa kutumia njia mbalimbali
zikiwemo ufadhili au matamasha ya muziki na starehe katika visiwa
hivyo. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman alisema
anakubaliana na maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuondoa kabisa
matangazo ya pombe na kwamba serikali imefanya vyema, kwani hivi sasa
Shirika la Afya Duniani WHO, Umoja wa Ulaya EU na baadhi ya nchi
ikiwemo Sweden tayari zimezuia matangazo ya pombe na Zanzibar kufuata
sheria hiyo ni jambo la busara.
0 comments:
Post a Comment