Na Millard Ayo
Baada ya Naibu waziri wa Elimu
na Mafunzo ya ufundi Philipho Mulugo kuomba radhi kwa wote waliomfikiria
vingine baada ya kuzungumza kwenye mkutano Afrika Kusini kwamba
Tanzania ni muungano wa Pemba na Zimbabwe msanii wa bongofleva Afande
Sele ametoa maoni yake.
Sele ambae ameahidi kugombea ubunge wa Morogoro mjini 2015 huku akisisitiza kwamba atakua kwenye chama pinzani na sio CCM namkariri akisema “ni jambo lisilofikirika licha ya dhamana ya uwaziri aliyonayo muheshimiwa Waziri inasikitisha, kitu kibaya ni kwamba yeye ni naibu Waziri wa elimu na hilo swala linahusiana na maswala ya kitaaluma, nchi imepata uhuru mwaka gani, imeingia kwenye muungano mwaka gani, imeungana na nchi gani”
“Inasikitisha kwa sababu ni waziri alafu ni Waziri wa Elimu na swala lenyewe linahusiana na swala la kielimu, kama waziri mwenye dhamana ya elimu anashindwa kutambua basi ndio maana wanasema kwamba mtandao mzima wa serikali yetu basi mara nyingi haufanyi kile ambacho watu wanategemea kwamba kingefanywa vizuri, ndio maana inasainiwa mikataba mibovu kwa sababu mtu anawekwa kwenye nafasi ambazo hakustahili kuwepo” – Afande Sele
“Hana taaluma, hana uwezo wa kuwa na cheo au mamlaka flani… anapewa kwa sababu ya undugu, urafiki pengine na wale wenye ngazi za juu zaidi ndio wanaochangia kuwa na aina ya mawaziri wa aina ya huyu naibu waziri anashindwa kujua tarehe ya kuungana kwa nchi yetu, kwa hiyo ni mmomonyoko ambao umeanzia juu ambapo ushindi wa yote ni kuivunja nyumba na kujenga upya… swala la kujua tarehe ya uhuru, tarehe ya muungano swala la utaifa kama hilo halihitaji kusema eti mashine iweke sawa au mashine igeuze hata ukikosea maandishi mimi siwezi kukosea kama wewe, hana upeo hana elimu hastahili kuwepo hapo alipo, hata mtoto kama mwanangu Tunda hawezi kukosea jambo kama hilo” – Afande Sele

0 comments:
Post a Comment