Recent Posts

Thursday, October 4, 2012

COMRADE SAMABALA AGOMBEA UENYEKITI WA UVCCM MKOA WA DODOMA

Posted by Unknown 11:34:00 PM, under | No comments


       Mwanasiasa na mwanzilishi wa group maarufu la Tanuru la Fikra katika mtandao maarufu wa facebook, hatimaye amefunguka na sera ambazo zitamwingiza kwenye cheo hicho chipya endapo kama wanachama wa Dodoma (UV-CCM) watamchagua katika kinyang'anyiro hicho. na haya ndio maneno yake kwenye ukurasa wa facebook

‎>----SAFARI NDEFU YA MAFANIKIO INAENDELEA-------->

*...SHUKRANI ZANGU KWA WOTE NINAOWAPENDA...*

Ndugu zangu wana TANURU LA FIKRA Na Watanzania wenzangu wote kwa Ujumla.

Jioni ya Leo napenda kuchukua fursa hii kusema Machache kwenu.:-

1. Kwanza Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyeniumba mimi na akaumba na vyote vilivyomo na mwenye Kumiliki kila kitu. Mfalme wa Wafalme.

2. Pili Napenda kuwashukuru zaidi Wazazi wangu wawili kwa Kunileta duniani, kunilea kimaadili KIIMANI na Kimazingira. Hayo yote ndio yamenifikisha hapa nilipo na kufahamiana na kila Mmoja.

3. Tatu napenda kuwashukuru zaidi walimu wangu toka ngazi ya awali mpaka Chuo kikuu kwa kunifundisha na kunilea kutaaluma.

4. Na nne napenda kuishukuru Kamati Kuu ya CCM (CC) na NEC Kwa busara walizotumia na hatmaye kuniteua kuwa Mgombea wa Mwenyekiti wa VIJANA DODOMA, Na NEC kupitia wilaya ya Chemba.

Kwa kweli wamenipa Heshima kubwa sana kama Kijana na Mtoto wa Masikini wa Kijijini nisiye wa Ukoo wa 'KIFALME' sitokani na Tabaka la Viongozi. Naahidi Kufanya Makubwa...

Nami Kama Sambala mtoto wa Mzee Unda wa Kijiji cha Mondo Naahidi kuilinda heshima hiyo kwa Kufanya Kampeni Kistarabu, na pia ntakapopata Ushindi basi Ntawatumikia walionipa Nafasi.

Mwisho Niwaombe wote muendelee Kuniombea na Kuniunga mkono kwa Hali na Mali ili kufanikisha ushindi wangu.

NAWAAHIDI VIJANA WENZANGU WA KITANZANIA NA DODOMA NA KONDOA/CHEMBA KUWA SITAAWANGUSHA.

NA PIA NAWAAHIDI NTAKITUMIKIA CHAMA NA UMMA NA SITAMTUMIKIA MTU KWA MATAKWA YAKE.

KWA PAMOJA TUTASHINDA..

''...ONE VOICE MANY VOTES FOR SAMBALA....''

VIJANA NGUVU YA CHAMA..

0 comments:

Post a Comment